Kuhusu

m-paper ni njia mpya ya kusoma magazeti na majarida uyapendayo kama yalivyo, ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kupitia simu yako ya mkononi (smartphone) au mtandao. Kwa watumiaji wa simu zenye android unaweza kupata m-paper android app kwenye playstore, kwa watumiaji wa iOS (iPhone na iPad) wanaweza kupata m-paper iOS app kwenye App Store na kwa watumiaji wa simu nyingine zenye uwezo wa internet pamoja na kompyuta aina zote wanaweza kusoma magazeti kupitia web app kwenye tovuti hii.

Kwa kutambua umuhimu wa habari kwenye maisha yako, tunakupa magazeti na majarida kwa nusu bei ya mtaani. Yaani kama gazeti linauzwa shilingi 800, utapata gazeti lile lile kwa shilingi 400 pekee. Furahia huduma zetu kupitia simu yako ya mkononi au kompyuta.