Kuhusu
 1. Je m-paper ni nini?
 2. m-paper ni njia mpya ya kusoma magazeti na majarida uyapendayo kama yalivyo, ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kupitia simu yako ya mkononi (smartphone) au mtandao. Kwa watumiaji wa simu zenye android unaweza kupata m-paper android app kwenye playstore, kwa watumiaji wa iOS (iPhone na iPad) wanaweza kupata m-paper iOS app kwenye App Store na kwa watumiaji wa simu nyingine zenye uwezo wa internet pamoja na kompyuta aina zote wanaweza kusoma magazeti kupitia web app kwenye tovuti hii
 3. Je m-paper ni BURE?
 4. Ndio, mfumo mzima wa m-paper pamoja na programu zake ni BURE. Magazeti na majarida yanayopatikana ndani ya m-paper huuzwa kwa nusu bei ya mtaani. Yaani kama gazeti linauzwa shilingi 500 kwenye kibanda cha magazeti, basi litauzwa kwa shilingi 250 kwenye m-paper.
 5. Je m-paper hutumia lugha gani?
 6. m-paper inapatikana kwa lugha mbili. Kiswahili na Kiingereza. Unaweza kubadili lugha kwa kubofya vitufe vilivyoandikwa lugha husika juu kulia.
 7. Je ni vifaa vipi vinaweza kutumika na m-paper?
 8. Kwa sasa unaweza kutumia programu ya m-paper kwenye simu zote zenye Android, iOS na kompyuta zote.
 9. Je kuna majaribio yoyote kabla ya kununua?
 10. Utakapojiunga kwa mara ya kwanza (kupitia namba yako ya simu) utapewa BURE magazeti matatu ili uweze kufanya majaribio.
 11. Je kuna majaribio yoyote kabla ya kununua?
 12. Utakapojiunga kwa mara ya kwanza (kupitia namba yako ya simu) utapewa BURE magazeti matatu ili uweze kufanya majaribio.
 13. Je ninawezaje kuanza kutumia m-paper?
 14. Kwenye computer au simu yako tembelea www.mpaper.vodacom.co.tz, ingiza namba ya simu, utapokea namba maalumu (code) za uthibitisho.
 15. Nawezaje kuongeza salio kwenye akaunti yangu?
 16. Unaweza kuongeza salio kupitia muda wa maongezi au MPesa. Kwa MPesa fuata hatua zifuatazo. 1. Piga *150*00# 2. Chagua 4 Lipa kwa M-Pesa 3. Chagua 3 Chagua kwenye orodha 4. Chagua 5 Vodacom 5. Chagua 4 M-Paper 6. Weka namba ya kumbukumbu (insert) 7. Weka kiwango 8. Weka PIN kulipa 9. Utapokea ujumbe wa udhibitisho wa malipo. 10. Bonyeza pakia tena kuona salio kwenye akaunti yako ya m-paper